Jinsi ya kupata simu iliyopotea: Android:






Simu hizo huwa moja wapo kati ya hizi: TECNO,  SAMSUNG  SONY,  na nyingine nyingi za aina hizi.

Kama simu yako iliyopotea ni android usiwe na wasiwasi. Hebu tufuatilie njia zifuatazo zinazoelezea kwa kina namna gani ya kuweza kuipata simu yako.


>>  Kwa kutumia  ANDROID DEVICE MANAGER (ADM)


Je, unatumia Google Play Store. Jibu lako bila shaka ni ndio na kama sio basi hakikisha umejiunga na Play Store. Kwa nini nimeanza na hili ni kwa sababu ili kujiunga na Play Store lazima uwe na akaunti ya Gmail. Kwa nini Gmail, kwa sababu hii ndiyo njia pekee itakayokuwezesha kutambua pahala simu yako ilipo. Android Device Manager ni programu ya google inayopatikana karibu katika kila smartphone ya android. Usijiulize maswali mengi na hata kama haujawahi kuiona usiwaze, hii hufanya kazi ndani ya smartphone yako. Jaribu kuisachi kama usipoipata unaweza kidownload kupitia Play Store au  bofya hapa.

Programu hii itatusaidiaje?
ADM hufanya kazi ya kutambua pahala simu yako ilipo kwa wakati husika endapo imeunganishwa na mtandao wa internet. ADM pia huweza kulock au kufuta simu nzima kama umeifanyia settings.  Kama simu yako imepotea au imeibiwa fanya yafuatayo ili kuipata.

  • Ni rahisi sana. Kama umetimiza yote hapo juu, punde tu unapogundua simu yako imepotea tafuta laptop/computer au simu ya android nyingine yoyote. Sign-in katika gmail kupitia kifaa hicho. Ukisha Sign-In tembelea tovuti ya ADM hapa. Au search tu google 'Android Device Manager' na chagua tovuti yao pale juu kabisa. 
  • Tovuti hiyo ikishafunguka utaweza kuchagua kifaa chako (Smartphone/Tablet) ambayo imeshajisajili kupitia e-mail yako 



  • Baada ya kuchagua Google itakuonesha ramani ya wapi simu hiyo ilipo. Baada ya hapo unaweza kuchagua kitufe cha ring. Hata kama aliyeiiba ameshabadili line simu hiyo itaita kwa muda wa dakika kama tano.



  • Zaidi pia ni jinsi ya kulock simu yako kupitia huduma hii hii ya ADM. Utaweza kufanya hivyo kwa kuchagua kitufe cha Lock. Kumbuka kitufe hiki kifanya kazi endapo ulifanya settings za kuruhusu ADM kulock na kufuta simu. Faida moja wapo pia ya kutumia option hii ya Lock ni kwamba unaweza kuandika ujumbe ambao yeyote mwenye simu hiyo kwa wakati huo ataiona.



  • Pia unaweza kufuta data zote zilizopo katika simu yako hiyo kama unahisi imeibwa au imepotea kabisa kwa kubonyeza kitufe cha Erase. 


Njia hii huweza kufanya kazi endapo tu, umeshajiunga na gmail, na pia simu iwe imeunganishwa na internet. Hii ndiyo njia bora kwa mujibu wangu. Usipofanikiwa mara ya kwanza endelea kujaribu usikate tamaa, kama mwizi ameiba smartphone lazima nyakati fulani ataingia tu katika mtandao. Akiingia tu basi kajichanganya. Ni vyema utoe taarifa polisi ni wajibu wao kuhakikisha usalama wako na mali zako.

Mlunda Rwanda

We all got 24 hours a day so you better use them well.