Maujanja ya ku-update Drivers za Kompyuta




Neno la kiswahili la driver ni dereva, hivyo hata katika kuiendesha Computer katika hali yake inayotakiwa lazima iwe ina madereva (drivers).


Driver ni programu inayoiwezesha Computer yako kuweza kuwasiliana vizuri na vifaa (hardwares) vinavyoiendesha hiyo kompyuta kama vile kadi ya video, printa na kadharika.Mifumo (windows) karibu yote inayotumika kuendesha kompyuta kwa kawaida huja na drivers zake ndani yake. Kutokana na kompyuta kuwa tofauti tofauti toka kampuni moja au nyingine, huja hitaji la kufunga driver nyingine au kuzibadili zilizopo ziwe za kisasa zaidi (update).
Katika somo hili tutajifunza namna ya ku-update au kufunga drivers mpya bila kutumia CD, unachohitaji ni kuwa na intaneti tu,

Baada ya hapo click >> start kisha andika device manager kisha utaona drivers zilizo na alama ya njano ikionyesha kama hatari, sasa unachotakiwa kufanya ni kubonyesha right click kwenye mouse yako au kwenye touchpad kama wewe ni mtumiaji wa laptop kisha utaona sehemu imeandikwa update driver... na ukishafanya hivo computer yako yenyewe itatafuta drivers mtandaoni, itazi-update na kisha kuziinstall kwenye computer yako ZINGATIA tafadhali kumbuka kua na internet yenye uhakika.
AHSANTE

Mlunda Rwanda

We all got 24 hours a day so you better use them well.