Maujanja ya kujua na kununua processor nzuri ya computer


Processor (prosesa) ndiyo ubongo wa computer, pia kuna processor katika simu na hata tablet. Kila kitu kinachofanyika kwenye computer yako lazima kipitie kwenye processor iwe ni kuandika maandishi kwenye computer, iwe ni kuperuzi intaneti iwe unaangalia video au chochote lazima kipitie kwenye processor. Na hii ndiyo sababu unaponunua computer unapaswa kuwa makini sana kujuwa ni aina gani ya processor iliyonayo hiyo computer.
Ni kwa namna gani processor ya computer hufanya kazi na kwanini aina ya processor iliyonayo computer ni kitu mhimu sana?
Uwezo wa computer kuhimili na kufanya kazi unategemea kwa sehemu kubwa na uwezo wa processor iliyonayo, processor ikiwa ndogo ndivyo na computer itakavyokuwa ikifanya kazi kivivu na kwa taratibu zaidi. Kumekuwa na mabadiliko ya processor kutoka toleo moja hadi linguine kila mara …Pentium D, Pentium M, Duo core na sasa tupo kwenye core i3, core i5, core i7 … ambazo ndizo processor zenye spidi kubwa zaidi.
Spidi ya processor hupimwa katika Megahertz (MHz) au Gigahertz (GHz). GHz 1 ni sawa na 1000MHz. Core 1GHz ya processor inao uwezo wa kumaliza kukokotoa billion 1 ya mahesabu kwa sekunde 1. Hii inawezakuwa ni kiasi kikubwa sana cha taarifa kuweza kufanyika katika kipindi cha muda mfupi sana, ingawa bila kutumia computer yenye processor ya kisasa hilo halitawezekana, unaweza ukaiamuru Computer kufanya kazi na ikakubidi uende nje ukapumzike kwanza kabla haijamaliza kufunguwa ukurasa mmoja wa intaneti.
Unapokuwa na Kompyuta yenye processor nzuri hii inamaanisha unaweza kufanya kazi nyingi kwa pamoja, unaweza ukawa unarekodi video kwenye DVD tupu huku unaperuzi intaneti au huku unasikiliza muziki na kadharika lakini kama ni ndogo kila mara unalazimika kusubiri imalize kazi moja ndipo uhamie nyingine. Hata hivyo lazima kujuwa ni kazi gani hasa unaenda kufanya na hiyo computer unayotaka kununua, kama ni kwa ajili tu kuandika makala, kusoma barua pepe na kutembelea mtandao tu wa intaneti basi processor ya kawaida itakutosha usije ukapoteza hela kununua computer yenye processor kubwa kumbe kazi zako ni kawaida tu.
La mhimu lingine kulijuwa kuhusu processor ni kuwa, tofauti na hard disc yaani kitunza kumbukumbu au memori kadi ya computer au RAM ambavyo unaweza kuvibadili muda wowote, mara nyingi processor ya computer huwa hazibadilishwi, kwa mfano computer iliyonunuliwa ikiwa na Pentium D kamwe huwezi kubadili na kuweka processor ya Duo core kwa sababu mifumo mingine iliyomo humo haiendani na ukubwa wa hiyo processor unayoongeza.
Wakati huo huo ni mhimu kutofautisha kati ya CPU (Central Processing Unit) na Processor. CPU inajumuisha vingi ikiwa ni pamoja na motherboard, processor yenyewe, RAM, Hard disc na kadharika.

Mlunda Rwanda

We all got 24 hours a day so you better use them well.